Marehemu
Jaji Khamisi (Kashi)
Habari
iliyotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa filamu nchini Jaji Khamis
(Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee
masinde,samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi
Amefariki
dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya muhimbili alikokuwa
amelazwa,akizungumza na the super stars tz raisi wa shirikisho la wasanii
amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga lakini
amedai yote ni kazi ya mungu
Nae mzee masinde ambaye alikuwa nae katika kundi moja
akiwa kama kiongozi wake amesema kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na
kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi)
mahali pema pepponi Amini.
No comments:
Post a Comment