Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.
H Baba akisaini kitabu cha ndoa.
Akizungumza na mwandishi wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua
kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa
dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana
wakaamua kufanya maulidi tu.
H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.
BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu
na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi,
wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu.
Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo,
uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa
sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.
Flora akimnywesha mumewe kinywaji.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa,
walio
ndoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na
sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.
No comments:
Post a Comment