Aminiel Aligaesha
ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba
msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya
kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za
kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua
anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwenye maelezo
aliyoyatoa kwa millardayo.com Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye
idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa
huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa
Mahututi na baadae kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment