Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus
akionyesha moja ya tuzo zitakaotolewa kwa wasanii sikuya Jumamosi kwenye ukumbi
wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya Steps
Solar, Johnson Mwamba.Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited Jumamosi
itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali waliopo
katika tasnia ya filamu Tanzania.
Mratibu wa
tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika kwenye
ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii wanaofanya
kazi na kampuni yao tu.
Silondwa
alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya Mwaka,
Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya
mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike, muigizaji bora wa kiume,
muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.
Silondwa
alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni kuleta
ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote kampuni
inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa
filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia
ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.
Alisema
kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali
ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi
kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima kwa waliotangulia
kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.
“Tunaamini
kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu kuongeza
ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza
na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha ambayo imekuwa
ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza na kuvuka
mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.
Alisema
kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa baadae, na
kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye mlengo wa
kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo kuwatumia wadhamini wa
nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps Solar pekee
Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba (mwenye koti)
akizungumzia udhamini wa kampuni yao katika tuzo za Steps Movie Award zilizopangwakufanyika
Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl.
No comments:
Post a Comment