Utabiri wa wengi kuwa ushosti
wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja
kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana,
“Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia
Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia,
unaambiwa hata salamu ikawa hakuna.
“Hapo ndipo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.
“Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.
“Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.
“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.
“Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.
TATIZO MILIONI 13?
“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?
“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala
alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7
jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?
“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?
“Hapo ndipo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.
“Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.
“Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.
“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.
“Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.
TATIZO MILIONI 13?
“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?
“Mimi nakwambia ndiyo maana ameamua kwenda kupumzika Mwanza baada ya kuwa wananuniana kwa kwenda mbele.”
Baada ya kupata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya kilongalonga chake cha kiganjani ili kupata undani wa sakata hilo lakini hakupatikana hewani.
Baadaye mwanahabari wetu alisaga lami hadi kwa staa huyo Kijitonyama, Dar, alipogonga geti alitoka mlinzi aliyedai kuwa ‘malkia’ alikuwa ndani amelala na hakuhitaji usumbufu pamoja na kwamba ilikuwa saa 6:30 mchana.
Hata hivyo, mwanahabari wetu alibisha hodi ofisini kwa Wema, Mwananyamala-Komakoma ili kuzungumza na meneja wake, Martin Kadinda ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu.

“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na
mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa
sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”
Alipoulizwa Wema anaumwa nini, Kadinda alifunguka: “Sijajua lakini ugonjwa ni siri kati ya mhusika na daktari, cha msingi wewe ujue tu anaumwa.”
Baada ya kupita kote huko kusaka undani wa sakata hilo, mwandishi alimgeukia Kajala kwa njia ya simu ya mkononi akiwa jijini Mwanza na kumuuliza kulikoni kutibuana na Wema.
Huku sauti ikiwa chini, Kajala alisema: “Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”

Chanzo: Gazeti la Ijumaa