Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la
Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu
mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa
Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013
akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu
Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la
Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee
hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili akimkabidhi mjumuisho wa michango
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude
katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe
iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini
Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro,
Mhashamu Telesphor Mkude wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na
kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja.
No comments:
Post a Comment