Msanii Noorah ameongelea mengi
kuhusiana na kwa nini yupo kimya sana katika game la muziki wa bongo..Noorah
ameyasema yake mengi wakati akihojiwa katika Kipindi cha Fleva GX ya Impact FM
ambapo alielezea hasa ukimya wake unatokana na nini.
Kikubwa zaidi Noorah alisema kwamba
toka kitambo alikuwa anafanya muziki lakini ndoto zake hazikuwa katika muziki
kama tulivokuwa tukidhania lakini aleweza kueleza kwamba ana ndoto zake tofauti
na Muziki ambazo zinamfanya akae kimya sana japo siku za hivi karibuni alitoa
track aliyomshirikisha msanii Alikiba.
Pia msanii Noorah aliweka wazi
kuhusiana na suala la Record Lebel kwa wasanii na studio za kibongo kwa kusema
kuwa kwa Bongo bado hakuna Studio ambao wanatimiza ile maana ya kuwa Lebel na
wasanii fulani kwa kudai kuwa hakina studio hata moja ambayo inakuwa tayari
kumhudumia msanii wake vitu mbalimbali akitolea mfano wa MATIBABU hasa pale
msanii husika anapoumwa. Kutokana na studio nyingi kuwa hazifanyi vitu kama
hivo kwa hapa Tanzania basi Noorah akasema bado hatuna Record Lebel hapa Bongo
zaidi ya kwamba wote ni wazugaji tu kwani hawatimizi yale yanayotakiwa
kufanywa. Alieleza hayo yote wakati alipoulizwa swali kwamba yeye yupo Lebel
gani kwa hapa Bongo...ndipo alipofunguka hayo..
No comments:
Post a Comment