Wednesday, March 27, 2013

[Audio & Lyrics] Brand New: Stamina ft. Fid Q - Wazo La Leo

Hapa chini mistari au mashairi ya wimbo huu, check jamaa walivyochana na bars za hatari...
Intro...
U know what majani?? Nice to meet you Homie
It's MORO Town Baby... SHOROBWENZI

Verse 1. (Stamina)
Elimika Nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo
Vaa uaminifu, tupa boksi la kondomu
Hip hop haijengwi na bifu, underground usijaze fomu
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe irizi
Viongozi msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
Mkulima rudi shamba, dec mbegu siku hizi hazioti
Maisha njia panda, mtembezi chagua pa kwenda
Uchumi vazi la bwanga, ukishuka uvishe suspenda
Shiba kwa nia, ukiwa mlafi wa malengo
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo
Punguza pupa, mpendaji uingie ndoani
Mapenzi yamevaa bukta, uswazi mapaja hadharani
Usilale kijinga, kwenye kitanda cha ushamba
Unaweza kuwa shabiki wa Simba,na ukaishi mwembe Yanga

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya, lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma, kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha, mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Verse 2. (Stamina)
Underground panga tenzi, u-star hauji kwa promo
Hakuna tajiri wa mapenzi, kapuku punguza ngono
Bora uitwe mfalme jua, kwenye utawala wa kishamba
Mapenzi yakikusumbua, tafuta daktari wa kitanga
Vazi unaloishi, mwenyezi yeye ndio designer
Shetani akikushawishi, mvute kwake kama dayna
Dunia duara, jitahidi uizunguke
Mla bata starehe hasara, wekeza hadhi isishuke
Huna undugu na bakhersa, niaje aje unakula unga
Mateja wanahitaji sensa, taifa la kesho linavunda
Dogo jifunze, heshima sio upaparazi
Mwambie na dada ajitunze, mlango wake asiuache wazi
Kama unajijua ni mchoyo, basi usingoje kupewa
Tafuta pesa kwa moyo, sio kwa ushindi wa ngekewa
Sharo mpe salamu, the great braza kanumba
Mwambie bongo sio tamu, na lulu bado wamemfunga

Chorus (fid Q)
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya, lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma, kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha, mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Verse 3. (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi, sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi, hata mle hadi mkasaza
Nchi tayari imekonda, mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba, kidonda anafanya mtaji
ukipata mazuri, jipange kuikwepa hasara
kijana vazi la msuli, haliwezi kukuvisha busara
ukiishi kwa hisia, kila stone litakubanza
cha msingi ni kuweka nia, ujivue kuwa mtanza
kata ya kijiji, haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mkwiji, msuli ukishuka kimeo
uchumi umeshika tama, kwenye shavu la mlanguzi
raia usilaumu chama, shiriki kwenye uchaguzi
unaweza ukavaa kinga, ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga, sambaza ujumbe wasifu
hakuna snitch kama pesa, ukiwa nae fanya vya maana
akiondoka atakutesa, utamsaka usiku na mchana

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya, lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma, kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha, mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Wednesday, March 20, 2013

ROSE NDAUKA SASA KUJA NA TV TALK SHOW



ROSE NDAUKA


CREW ya KIKOI 

ON SET YA THE FAMILY TALK SHOW
BAADA YA KUFANYA MAONGEZI YA KINA YA MIGOGORO YA NDOA YA SAM WA UKWELI

Sunday, March 17, 2013

SAMWELI HAIR CUTS SALON (DODOMA-Bonanza area)


SAMWELI HAIR CUTS SALON (DODOMA-Bonanza area)
Quality with the greater competitive prices,
You are warmly welcome
FOR MORE INFORMATION CONTACT
Saloon Keeper (SK)
Samwel Mwakalambo
Tell 0715 150 868
Email samwel.mwakalambo@yahoo.com
http://www.facebook.com/samwel.mwakalambo

Saturday, March 16, 2013

Sasa inapatikana sokoni.Usingoje kusimuliwa.


Bongo Move,Sasa Zinapatikana sokoni, Mahitaji ya oda piga simu +255754260419









NEW MAISHA CLUB..!! Usikose...!!!


Friday, March 15, 2013

FILAMU YA KISWAHILI YATENGENEZWA INDIA

Gray nerve films is a movie production company which started at 2011 with a vision of turning around the Bongo movie era into something much more elegant .this all idea started with a group of 3,Daniel,Zabron and Tom jimmy but we had no idea if someday a company will emerge out of our hard work.

We the people who started the company had to go separate ways since others were done with university programs today 3 people own the shares of this production company Joseph Raphael, Daniel Mgopa and Timothy. 
 
We have been successful in collaborating with different people and companies such as HOME STUDIOS and OJ PRODUCTION; we shot our first benchmark movie as graynerve films on 2012 January and it was released in late December and we are still on board cause we never run out of ideas.

 
 

Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred

Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akiwa na Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushilla Thomas.
 
 
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (tatu shoto) akiwa na baadhi ya washiriki wenzake wa Miss Tanzania mwaka jana.
 
 
 Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini wakuu wa Shindano la Miss Tanzania,Kushilla Thomas (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party),iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam

 Mapumziko mafupi Baada ya dansi.

 Hii ndio Kamati nzima ya Miss Tanzania.


Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga akizungumza machache wakati wa wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party) ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14,iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
 
 Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akiwa katika picha pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro (kushoto) na Meneja wa vilaji vha Castle Lite na Ndovu,Pamella Kikuli wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party) ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14,iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam

Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro (kati) akiliongoza Dimba kwa kusakata kwaito.
 
Hapa hakuna alietaka kubaki nyuma kwa magoma yalipamba moto na kila mtu aliyarudi bila kujali nin wala nini.

RAIS KIKWETE ASHIRIKI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIGURUNYEMBE,MOROGORO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013 akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili akimkabidhi mjumuisho wa michango Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja.