Friday, February 22, 2013

RAIS WA KENYA, MWAI KIBAKI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA

Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiwa na maofisa mbalimbali wakiondoka Kiwanda cha Magereza Ukonga baada ya kumaliza kuangalia vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.


 Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya  Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.


Mshauri Mtaalamu wa Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu katika Jeshi la Magereza, Alpherio Moris (kulia) akimuonyesha Rais Mwai Kibaki moja ya kofia ngumu (Helmet) ambayo inatarajiwa kutengenezwa na kiwanda cha magereza Ukonga hivi karibuni.



Rais Mwai Kibaki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali nchini pamoja na maofisa kutoka nchini Kenya.


No comments: