Sunday, June 9, 2013

Kilimanjaro Premium Lager


.Wimbo Bora wa Mwaka Hip Hop...... ni Dear God wa Kala Jeremiah




Chalz Baba akiwa na Tuzo zake!
 
Ommy Dimpoz kwa mara nyingine tena! Tuzo ya Video Bora ya Mwaka..Baadae!

Burudani ya kutosha katika Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.

 Ben Pol akiwa kwenye stage na tuzo yake ya Mtunzi Bora wa Mashahiri Bongo Fleva.




TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Marakech mjini hapa na wenyeji Morocco, katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani. Hadi mapumziko, Morocco walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Abderazak Hemed Allah dakika ya 37, baada ya yeye mwenyewe kujiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kugongana na Aggrey Morris. Morris alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya hapo na Stars wakabki pungufu. Kipindi cha pili Morocco walirejea na moto tena, wakiishambulia zaidi Stars iliyoonekana kudhoofika na katika dakika ya 50 Youssef El Arabi akafunga bao la pili kiulaini baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania na kubaki na kipa Juma Kaseja.
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza liliipatia Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager bao la kwanza dakika ya 61 lililofungwa na Amri Kiemba kwa shuti la mbali kutoka wingi ya kushoto. Kwa matokeo hayo, Stars inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi nne, kushinda mbili nyumbani na kufungwa mbili zote ugenini, nyingine ikiwa dhidi ya Ivory Coast.
Lakini Stars inabaki nafasi ya pili mbele ya Morocco yene pointi tano sasa, wakati Ivory Coast wanaongoza kwa pointi zao saba kabla ya matokeo ya mechi na Gambia leo.

R.I.P ALBERT MANGWEA..!!!



Saturday, May 11, 2013

UK TOUR:HILI NDIO VAZI ALOVAA DIAMOND KWENYE SHOW JANA MJINI READING


Hi ni picha ya super star Diamond aliwekaa jana kwenye
mtandao wake wa Instangram
akiwa amejitayarisha swadakta kabisa kwenda
kushambulia jukwaa.....pamoja na
dancers wake pichani awapo...!!

Dress code hiyo ya Kinyama ambayo imedizainiwa na vijana
machachari kutoka Bongo land
Twinsfashion Akufunguka kuwa gharama yake,
Lakini ni ya kinyama sana....!!

More Info About Diamond Platnumz;Follow Him On
Instangrama By DiamondPlatnumz,On Twitter By
@Diamondplatnumz,On Facebook By Diamond Platnumz
and u can also connect with Him
By His Fan Page Goes By Diamond Platnumz............

LAURYN HILL AFUNGWA JELA! KISA ...........

Baada ya kushindwa kulipa deni la kodi la dola milioni 1 ndani ya wakati aliokuwa amepewa na mahakama, Mwanamuziki mwenye rekodi ya kushinda tuzo za Grammys, Lauryn Hill amehukumiwa kifungo cha miezi 3 jela.

Mbali na kukomaa na kulipa kiasi cha dola laki 9, zaidi ya shilingi bilioni 1 na milioni 400 za kitanzania mpaka juzi, ili kujaribu kujiokoa na kitanzi, Deni la mwanadada huyu bado lilionekana kumuelemea hasa kutokana na riba na faini ambazo ziliongezeka katika madeni yake ya muda mrefu.

Hill kwa sasa anajipanga kujirudisha tena katika game ya muziki na kwa mujibu wa hukumu anatakiwa kuripoti gerezani tarehe 8 mwezi July kwaajili ya kuanza kutumikia kifungo chake.

SIR ALEX FERGUSON KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU

Manager wa timu ya uingereza Manchester United, Alex Ferguson
anatarajiwa kustaafu baada ya kufanya kazi na timu hiyo kwa
zaidi ya miaka 30,club hiyo imetangaza jumatano ya leo

Ferguson mwenye miaka 71 hivi sasa amefanikiwa kusimamia timu hiyo yenye mamilioni ya mashabiki tangu mwaka 1986
katika miaka yaje 26 kama manager wa timu hiyo, alishinda vikombe 30 pamoja na vikombe vikubwa 13
Ferguson ataachia nafasi hiyo baada ya game ya mwisho ya club hiyo kwa msimu huu ambayo itakuwa ni mechi kati yao na Manchester City
haijajulikana bado nani atakae mrith kiti hicho