Saturday, May 11, 2013

LAURYN HILL AFUNGWA JELA! KISA ...........

Baada ya kushindwa kulipa deni la kodi la dola milioni 1 ndani ya wakati aliokuwa amepewa na mahakama, Mwanamuziki mwenye rekodi ya kushinda tuzo za Grammys, Lauryn Hill amehukumiwa kifungo cha miezi 3 jela.

Mbali na kukomaa na kulipa kiasi cha dola laki 9, zaidi ya shilingi bilioni 1 na milioni 400 za kitanzania mpaka juzi, ili kujaribu kujiokoa na kitanzi, Deni la mwanadada huyu bado lilionekana kumuelemea hasa kutokana na riba na faini ambazo ziliongezeka katika madeni yake ya muda mrefu.

Hill kwa sasa anajipanga kujirudisha tena katika game ya muziki na kwa mujibu wa hukumu anatakiwa kuripoti gerezani tarehe 8 mwezi July kwaajili ya kuanza kutumikia kifungo chake.

No comments: