Saturday, May 11, 2013

CONGO NDIO NCHI NGUMU ZAIDI DUNIANI KULEA WATOTO


Shirika la Save the Children, limeeleza kuwa, Jamhuri ya
 Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa ndio nchi ngumu zaidi
duniani kulea watoto.
Nchi ya Finland imetajwa kuwa sehemu bora duniani kuwa 
mama, huku Sweden na Norway zikifuatia katika nafasi ya pili na tatu.
Shirika hilo la hisani limetumia vigezo vya huduma ya afya
 kwa akina mama, vifo vya watoto, elimu na kipato 
katika nchi 186 duniani kutoa takwimu hizo.
Nchini India, zaidi ya watoto 300,000 hufariki dunia saa 24
 baada ya kuzaliwa, hivyo kuchangia 29% ya vifo vya watoto 
wanaozaliwa duniani kote imeeleza ripoti ya shirika hilo.
Nchi kumi zilizoshika nafasi ya mwisho zote zinatoka eneo la 
Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako kwa wastani, mwanamke 
mmoja katika 30 hufariki dunia kutokana na matatizo ya ujauzito 
na mtoto mmoja kati ya saba hufariki kabla ama baada ya 
kufikisha umri wa miaka mitano.
Nchini DRC, vita na umasikini vimewaacha akina mama wakiwa
 dhoofu kiafya na bila msaada wowote hasa wakati wa hatari 
kubwa katika maisha yao.
Nchi nyingine zilizotajwa kuwa hatari ni Somalia, Sierra Leone, 
mali, Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gambia, Nigeria, 
Chad na Cote D’Ivoire.
Shirika hilo la hisani limesema, ukosefu wa lishe bora ni 
sababu kubwa ya kuongezeka kwa idadi ya vifo vya akina 
mama na watoto wachanga katika nchi za Kusini mwa Jangwa la 
Sahara, huku 10% - 20% ya akina mama wakiwa hawana 
uzito unaostahili.
Kinyume chake, matokeo hayo yanaonesha kuwa, Finland ni nchi 
bora kuwa mama, huku hatari za vifo vitokanavyo na ujauzito 
ikiwa ni moja kati ya akina mama 12,200 na watoto katika 
nchi hiyo wakihudhuria karibu miaka yote 17 ya elimu ya awali.
Sweden, Norway, Iceland na Uholanzi zilikuwa pia miongoni
 mwa nchi bora 10, ambapo Marekani iko nyuma katika nafasi ya 30.
Lakini jambo la kustaajabisha, ripoti ya shirika hilo imebaini
 kuwa, Marekani ina kiwango cha juu cha vifo vya watoto 
wanaozaliwa katika nchi zenye viwanda duniani, ambapo
 watoto 11,300 hufariki dunia katika siku wanayozaliwa kila mwaka.
Shirika hilo limesema, hali hiyo inasababishwa na idadi kubwa 
ya watu nchini Marekani pamoja na wingi wa watoto wanaozaliwa
 kabla ya wakati. Marekani ni miongoni mwa nchi zenye kiwango 
cha juu cha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ikiwa na uwiano 
wa mtoto mmoja kati ya wanane.
Ipoti hiyo imegundua kuwa, akina mama na watoto hufariki dunia
 kwa idadi kubwa huko Kusini mwa Asia kuliko eneo lolote duniani, 
ikikadiriwa kuwa, watoto 423,000 hufariki dunia siku 
wanayozaliwa kila mwaka.
India imetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya watoto 
wachanga,(ikiwa ni 29% ya vifo duniani) na pia vifo vingi vya 
akina mama kuliko nchi yoyote duniani ambapo akina 
mama 56,000 hufariki kila mwaka.habari kutoka BBC

No comments: