Saturday, October 20, 2012

Rihanna atumia jina la album yake kuwajibu walioiponda picha yake ya kwenye cover ya album hiyo.


Baada ya Rihanna kureveal cover ya studio album yake ya saba yenye jina “Unapologetic” watu wengi walitoa maoni kupitia mitandao ya kijamii kama facebook na twitter.

Album cover hiyo inayomuonesha Rihanna akiwa hajavaa chochote juu (naked), picha hiyo inaambatana na maandishi mengi kwenye mwili wake ambayo hayaeleweki japo mawili matatu yanaweza kusomeka lakini bado hayatoi picha inayoeleweka haraka. Kiasi cha kufanya fans wahisi labda ni majina ya nyimbo zitakazokuwa katika album yake, likiwemo jina ‘diamond’ na Unapologetic ambalo ndilo jina la album.

Katika picha ya album cover hiyo chuchu moja ya Rihanna imefunikwa na maandishi wakati nyingine ikiwa ameifunikwa na kiwiko chake cha mkono wa kushoto.

Watu wengi walitoa maoni mbalimbali baada ya kupata details za album hiyo ambayo inategemewa kuachiwa rasmi November 19, 2012 na wengi walionesha kusifia sana cover yake hasa ile picha na baadhi ya tweet za fans zilikuwa na maneno kama ‘I love that’, unapologetic sounds good‘ I’m so proud of her the cover and the name are totally Epic, Perfect, flawless etc’, na mengine mengi ya kusifia.

Lakini kuna walioponda na kushangaa hiyo cover iliyowekwa na wengine ikaonekana kama hii ni picha inayoonesha bad girl Rihanna ambae ni unapologetic.


Rihanna alionekana kutowajali ambao wameiponda na  aliamua kutumia maneno hayo hayo yaliyo kwenye cover la album akajibu critique za wasikilizaji kwa tweet “it's okay! Refer to: album title", akimaanisha she is unapologetic.



NEW VIDEO: MABESTE FT. JUX - SIRUDI TENA  


 
Tazama video mpya ya msanii Mabeste aliyomshirikisha Jux.

EXCLUSIVE: NEW VIDEO: C-SIR MADINI - PAIN KILLER (Official Music Video) HD version

 
C-sir Madini 
 Baada ya kuonyesha uwezo wake kupitia wimbo wake wa kwanza wa "Kifungo Huru" alioutoa mwaka jana 2011, uliofuatiwa na wimbo wake wa pili alioutoa January mwaka huu 2012 unaoitwa "Nishike Mkono", hii ndio single yake ya tatu ambayo kwa mara ya kwanza Leotainment inakupa nafasi ya kuiona video yake mpya aliyoipa jina la "PAIN KILLER"
Wimbo huu umeandikwa na kua produced na Kid bwoy wa Tetemesha Recordz. Video imesimamiwa na Adam Juma wa Visual Lab/Next Level.
Kwa mujibu wa management ya C-sir video itaanza kuonekana katika vituo vya TV mapema wiki Ijayo, na itaanza kusikika katika vituo vya radio wiki moja baada ya kuanza kuruka katika Tv stations.

 Kuwa wa kwanza kuitazama hapa

 





 

No comments: