Mwanamuziki
gwiji nchini Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa
toka kwa familia yake zinasema Bi Kidude aliekuwa akipatiwa matibabu katika
hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki
mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na
aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa
mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya
nguzo
kubwa.
No comments:
Post a Comment