"NIMEANDAA FILAMU MPYA AMBAYO NITAMSHIRIKISHA LULU MICHAEL"....JACKLINE WOLPER
MSANII
wa filamu Tanzania Jackline Wolper ameandaa filamu mpya
atakayoshirikiana na msanii maarufu Elizabeth Michael 'Lulu'
itakayokamilika hivi karibuni baada ya msanii huyo kutoka gerezani kwa
dhamana
Akizungumza na Maisha Wolpa alisema amepata faraja baada
ya taaratibu na sheria kufuatwa na hatimaye Lulu kuweza kupata dhamana
hivyo anatarajia kufanya naye kazi ya filamu mpya itakayoanza kurekodiwa
baada ya msanii huyo kufika uraiani
Alisema kuwa anatarajia
atafanya vizuri katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa akifanya
vizuri katika tasnia hiyo ya uwigizaji kabla ya kupatwa na matatizo
"Nimeshampokea
Lulu tangu moyoni mwangu kwani kule alikokuwepo si sehemu nzuri na
ukiangalia bado ni mtoto mdogo hivyo inaumiza sana" alisema Wolper
Filamu hiyo ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuchezwa na Lulu baada ya kufika Uraiani
Wakati
huo huo Rose Ndauka alisema ni wakati wa wasanii kumpokea mwenzao kwani
wote ni familia moja na wanahitaji kushirikiana katika kila hali
Alisema
kuwa ukiangalia umri wa msanii huyo ni mdogo hivyo ananafasi kubwa bado
ya kutengeneza maisha yake na kuangalia wapi amekosea na wapi anapaswa
kurekebisha
Naye msanii Single Mtambalike 'Richie Richie' alisema
anashukuru kuona sheria imechukua mkondo wake na hatimaye sasa ameweza
kuachiwa kwa dhamana hivyo kwa upande wao ni faraja kubwa kwani wote ni
familia moja
Alisema anaamini sasa ataweza kujipanga na kufanya
kazi vizuri kwani anakipaji na bado wanamuhitaji watanzania kulingana na
uwezo mkubwa alionao kwenye tasnia hiyo
No comments:
Post a Comment