Saturday, February 23, 2013

MASTAA WAKALI WA BONGO (DADAZ..!!!)

 Wema Sepetu (actress/former miss Tanzania)

 Vanessa Mdee (Mtangazaji/Msanii)

 Salma Msangi (Mtangazaji)

 Jackie Cliff (model)

Hamisa (model)


 Bridgitte Alfred (Miss Tanzania 2012)
 Millen Magese (former miss Tanzania)

 Jokate Mwegelo (presenter/fashion designer)


 Teddy Kalonga (model)
 Mange Kimambi (creative director)

Penny Mungilwa (Mtangazaji)


 Jackline Ntuyabaliwe aka kylin (Former Miss Tanzania) na msanii wa bongo fleva

Sintah (Actress)  

MWANAMZIKI WA HIP HOP JCB AFUNGA NDOA NA MZUNGU WAKE


JCB akidondosha  wino kwenye kitabu cha Ndoa..!!


  Msanii wa hip hop kutoka kundi la watengwa ambalo Maskani yake yapo Arusha  JCB Juzi aliuaga ukapela na Kufunga Ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Diana Jorgensen pande za Arusha..!!
 

Diana akidondosha  wino kwenye kitabu cha Ndoa..!!




Picha ya Pamoja ya JCB na Mkewe Diana wakiwa na Ndugu,Jamaa na Marafiki bahada ya kufunga ndoa..!!

RAPPER WIZ KHALIFA NA AMBER ROSE WAPATA MTOTO WA KIUME....!!


Amber Rose  na mchumba wake Wiz Khalifa  sasa ni wazazi wanaojivunia  kwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume.Sebastian Taylor Thomaz (yes, ikiwa na  a z mwisho) amezaliwa siku ya  jana alhamis mchana Mapema siku hiyo ya jana a proud papa Wiz Khalifa alipost picha akiwa amevaa posted a picture wearing scrubs na   face mask na maelezo yaliyokuwa yakisema  "daddy time."  wakati wa baba mida ya saa nane mchana akipost, "Happy Birthday Sebastian "The Bash" Taylor Thomaz!!!  Everyone welcome this perfect young man into the world"mara ya mwisho wawili hao. Amber na Wiz, walionekana katika tuzo za grammy, wikii mbili  zilizopita, huku rose akionekana na tumbo lake kuuuubwa katika tight dress nyeusi 

 



Friday, February 22, 2013

TATHIMINI YA JUMLA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012.

Kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani, waliofaulu ni 126,847 (daraja i-iv)
daraja I- 1,641 (0.4%)
daraja II- 6,453 (1.6%)
daraja III- 15,426 (3.9%)
daraja IV- 103,327 (26.0%)
daraja 0- 240,903 (60.7%)
sasa wanaoweza kwenda form 5 na 6 ambao ni kuanzia daraja la I-III jumla yao ni 23,520 (elfu ishirini na tatu mia tano na ishirini) kati ya wanafunzi 397,136 (laki tatu tisini na saba elfu mia moja thelasini na sita) hii ni sawa na 5.9224%.

Lowassa amtaka JK kuunda tume na Waliofeli wapanga kuandamana kumng’oa

WAKATI mjadala wa kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne ukiendelea nchini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume kuchunguza na kutoa mapendekezo ya mfumo bora wa elimu nchini.
Alisema kwa hali ilivyo sasa mtu mmoja hawezi kujifungia ofisini peke yake na kuja na mfumo wa kuboresha sekta ya elimu utakaokidhi matakwa ya jamii.
Lowassa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.
Ingawa hakutaka kuzungumzia hoja ya mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia (NCCR- Mageuzi), aliyetaka Bunge liunde kamati kuchunguza udhaifu katika sekta ya elimu na hoja hiyo kutupwa, Lowassa alisema hakuna sababu ya kubishana kama tuna mitaala au la, lakini jambo la msingi ni kuhakikisha tunapata sababu za matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne.
“Sitaki kuzungumzia mjadala wa bungeni huyo anasema hatuna mitaala, serikali inasema tunayo, hoja ya msingi zaidi ni kuangalia hii mitaala ni sahihi, inatufaa? Mfumo wetu wa elimu ni mzuri?” alisema Lowassa na kuongeza kuwa tume itakuja na majibu kama mitaala yetu ni sahihi na kama inatufaa au la.
Akitolea mfano, Lowassa wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, Waziri wa Elimu wakati huo, marehemu Jakson Makweta, aliunda tume kuchunguza mfumo wa elimu na ilikuja na majibu mazuri yaliyofaa kwa wakati ule na sasa tunahitaji tume nyingine kuja na majibu ya wakati uliopo.
“Miaka ya nyuma, Rais Reagan wa Marekani wakati huo, aliunda tume kuchunguza ubora wa elimu inayotolewa nchini mwake na tume hiyo ilikuja na majibu yaliyofanyiwa kazi na leo hii Marekani ina mfumo mzuri na bora wa elimu,” alisema Lowassa.
Alisema matokeo ya kidato cha nne mwaka huu, yanasikitisha na kama taifa lazima tupate sababu za hali hiyo na kutafuta ufumbuzi.
Alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kuwa ni pamoja na kuangalia namna gani serikali inawaangalia walimu kwa maana ya mishahara na mazingira yao ya kuishi wawapo kazini.
“Matokeo ya kidato cha nne yamenisikitisha sana maana asilimia 60 ya wanafunzi kupata ziro ni jambo la hatari. Na napenda kumsihii Rais Kikwete kwamba amefanikiwa sana katika sekta nyingine kama barabara, aunde tume kuchunguza sababu za wanafunzi kufeli, lakini kubwa kuliko zote tume hiyo ije na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mfumo wetu wa elimu,” alisema Lowassa.
Alisisitiza kuwa hoja ya kutaka serikali iunde tume kuboresha mfumo wa elimu, alipata kuitoa mara kadhaa kwani anaamini Elimu Kabla, Kilimo Kwanza.
“Kila Mtanzania anasema lake, wengine wanasema ni hujuma, wengine wanadai kuna mgomo baridi wa elimu, malalamiko na sababu ni nyingi na njia pekee ya kujua ukweli ni kupitia tume,” alisema Lowassa.
Akizungumzia shule za kata alizoziasisi nchini nzima, alisema anajivunia uwepo wa shule hizo hasa kutokana na mwitikio ambao wananchi waliuonyesha wakati anazianzisha.
Alisema matatizo na changamoto zinazozikabili shule hizo ni bora zikatafutiwa ufumbuzi kupitia tume anayopendekeza ianzishwe.
Alisema shule hizo ni mkombozi kwa wananchi wanyonge na zimeleta usawa na ni jambo la kujivunia kwamba ziko kwenye kila kata nchini.
“Hata hivyo kasi ya kuzihudumia shule hizo hatua kwa hatua imepungua na sitaki kumlalamikia mtu, lakini ni bora zikaendelezwa kwa kukabiliana na changamoto zake.
Mbali ya kuzungumzia anguko la elimu, Lowassa pia alizungumzia vurugu za kidini zinazoendelea nchini, hususan kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini visiwani Zanzibar.
Aliwasihi Watanzania kutambua kuwa amani iliyopo ina maana kubwa kwani zikianzishwa vurugu za kidini hakuna atakayebaki salama na hakutakuwa na mshindi.
Wakati huohuo, Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), limeitaka serikali kutangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyotoka hivi karibuni kuwa janga la kitaifa kwa lengo la kuliepusha taifa na fedheha ya kuzalisha kizazi cha watu wasiosoma.
Mbali na kutaka matokeo hayo kutangazwa kuwa janga la kitaifa, pia baraza hilo limesema limeshaanza kuwasiliana na vijana waliofeli kutoka maeneo mbali mbali ya nchi kwa ajili ya kuandaa maandamano ya kumtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA), Dk Joyce Ndalichako, na Mkaguzi wa Elimu ya Sekondari nchini, waachie nafasi zao kwa madai kuwa wameshindwa kusimamia majukumu yao.
Kauli hiyo iltolewa jana jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu BAVICHA, Deogratius Mushi, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kusikitishwa kwao na matokeo ya mitihani hiyo yanayoonyesha asilimia 60 ya wanafunzi, wamepata ziro.
Mushi alisema sababu kuu ya matokeo mabaya ni udhaifu wa serikali kushindwa kusimamia majukumu yake na kuchukulia kila jambo kwa wepesi.
“Hii serikali dhaifu ya CCM, mwaka 2006 ilisema lengo ni kufikia ufaulu wa asilimia 70 wakati huo tukiwa katika asilima 34 leo hata hiyo haipo sasa tunakwenda wapi na jeshi hili kubwa ambalo litakuwa haliajiriki tena kwa kukosa hata sifa ya kuwa na vyeti vya sekondari!?” alisema Mushi.
Katika hatua nyingine kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi waliofeli kutasababisha shule na vyuo vingi kukosa wanafunzi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa kuzungumza na wataalamu wa elimu unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi watashindwa kujiunga na masomo ya juu pamoja na vyuo.

RAIS WA KENYA, MWAI KIBAKI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA

Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiwa na maofisa mbalimbali wakiondoka Kiwanda cha Magereza Ukonga baada ya kumaliza kuangalia vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.


 Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya  Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.


Mshauri Mtaalamu wa Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu katika Jeshi la Magereza, Alpherio Moris (kulia) akimuonyesha Rais Mwai Kibaki moja ya kofia ngumu (Helmet) ambayo inatarajiwa kutengenezwa na kiwanda cha magereza Ukonga hivi karibuni.



Rais Mwai Kibaki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali nchini pamoja na maofisa kutoka nchini Kenya.