Saturday, October 27, 2012

KUTANA NA MISS MIRIAM NTAKISIVYA ALIYEJIKITA KUBUNI MAVAZI BAADA YA KUSHINDWA KTK KINYANG'ANYIRO CHA MISS TMK 2012 iii





  JINA KAMILI NI:-  Miriam Ntakisivya
UMRI:- (21 )
ELIMU :- Chuo
HOBIES:- Mwanamitindo, Burudani
MATARAJIO:- Kuwa mbunifu na Mwanamitindo wa kimataifa
ANAPATIKANA KATIKA:- kijamii  kama facebook Na Twetter kwa jina la Riam Ntakisivya
MAVAZI HAYA PICHANI: Ameyabuni yeye mwenyewe
NDOTO ZAKE:- Ni Kufanya vizuri na kufika mbali






Saturday, October 20, 2012

Rihanna atumia jina la album yake kuwajibu walioiponda picha yake ya kwenye cover ya album hiyo.


Baada ya Rihanna kureveal cover ya studio album yake ya saba yenye jina “Unapologetic” watu wengi walitoa maoni kupitia mitandao ya kijamii kama facebook na twitter.

Album cover hiyo inayomuonesha Rihanna akiwa hajavaa chochote juu (naked), picha hiyo inaambatana na maandishi mengi kwenye mwili wake ambayo hayaeleweki japo mawili matatu yanaweza kusomeka lakini bado hayatoi picha inayoeleweka haraka. Kiasi cha kufanya fans wahisi labda ni majina ya nyimbo zitakazokuwa katika album yake, likiwemo jina ‘diamond’ na Unapologetic ambalo ndilo jina la album.

Katika picha ya album cover hiyo chuchu moja ya Rihanna imefunikwa na maandishi wakati nyingine ikiwa ameifunikwa na kiwiko chake cha mkono wa kushoto.

Watu wengi walitoa maoni mbalimbali baada ya kupata details za album hiyo ambayo inategemewa kuachiwa rasmi November 19, 2012 na wengi walionesha kusifia sana cover yake hasa ile picha na baadhi ya tweet za fans zilikuwa na maneno kama ‘I love that’, unapologetic sounds good‘ I’m so proud of her the cover and the name are totally Epic, Perfect, flawless etc’, na mengine mengi ya kusifia.

Lakini kuna walioponda na kushangaa hiyo cover iliyowekwa na wengine ikaonekana kama hii ni picha inayoonesha bad girl Rihanna ambae ni unapologetic.


Rihanna alionekana kutowajali ambao wameiponda na  aliamua kutumia maneno hayo hayo yaliyo kwenye cover la album akajibu critique za wasikilizaji kwa tweet “it's okay! Refer to: album title", akimaanisha she is unapologetic.



NEW VIDEO: MABESTE FT. JUX - SIRUDI TENA  


 
Tazama video mpya ya msanii Mabeste aliyomshirikisha Jux.

EXCLUSIVE: NEW VIDEO: C-SIR MADINI - PAIN KILLER (Official Music Video) HD version

 
C-sir Madini 
 Baada ya kuonyesha uwezo wake kupitia wimbo wake wa kwanza wa "Kifungo Huru" alioutoa mwaka jana 2011, uliofuatiwa na wimbo wake wa pili alioutoa January mwaka huu 2012 unaoitwa "Nishike Mkono", hii ndio single yake ya tatu ambayo kwa mara ya kwanza Leotainment inakupa nafasi ya kuiona video yake mpya aliyoipa jina la "PAIN KILLER"
Wimbo huu umeandikwa na kua produced na Kid bwoy wa Tetemesha Recordz. Video imesimamiwa na Adam Juma wa Visual Lab/Next Level.
Kwa mujibu wa management ya C-sir video itaanza kuonekana katika vituo vya TV mapema wiki Ijayo, na itaanza kusikika katika vituo vya radio wiki moja baada ya kuanza kuruka katika Tv stations.

 Kuwa wa kwanza kuitazama hapa

 





 

Wednesday, October 10, 2012

August Movies....!!!!


Ndoa Yangu release Announcemrnt


Monday, October 8, 2012

BENDIZZO ENTERTAINMENT: OMMY DIMPOZI- BAADAE

BENDIZZO ENTERTAINMENT: OMMY DIMPOZI- BAADAE

OMMY DIMPOZI- BAADAE

                                            
   Msanii wa kizazi kipya Ommy Dimpozi , azidi kung'aa kimataifa baada ya  video yake mpya ijulikayo kwa jina la Baadae,

Sunday, October 7, 2012

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA FIESTA 2012 DAR WITH RICK ROSS


 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini




 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani  usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.




Mtu mzima Rick Ross “The Boss” kutoka nchini Marekani hivi sasa yuko jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar salaam ,anakamua ile mbaya na mashabiki wamepagawa vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika mbaya, hiii ni mara yake ya kwanza kufanya onesho nchini Tanzania 
  



GARI ALILOKUJA NALO RICK ROSS BONGO  




Rachel na wacheza shoo wake wakiburudisha mashabiki viwanja vya Leaders jijini Dar es salaal katika tamasha la Serengeti 





Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba Boy akiimba jukwaani usiku huu 

Saturday, October 6, 2012

I-View Studios Kusimamia Kazi za Diamond Platnumz

Platnumz akibadilishana mkataba na I-Views


CHINI: Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto)na msanii Diamond Platnumz wakisaini mkatabawa kufanya kazi pamoja. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole
 
JUU: Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo  na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.


DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane I-View.

“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana nay eye kinapaswa kupitia I-View,” amesema.

Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, lakini I-View pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba ndani na nje ya Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo.

Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika kumfanya aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.

“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na wanawasiliana na menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.

Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanuyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video hiyo.

I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.
Platnumz akidondoka mkataba na Menejiment ya I-View Studios





Wednesday, October 3, 2012

BAADA YA PRINCIPELS OF WOMAN SASA NI WAKATI WA SISTER MARRY



Baaada ya sinema ya Woman of Principels kufanya vizuri sokoni sasa ni wakati wa sinema bora kuingia mtaani jina ni Sister Marry ni sinemma yenye story ya kipekee sana kama kawaida ya kampuni yako RJ Company kufanya kazi yenye kiwango cha hali ya juu lini mzigo huu unatoka nitawataalifu kupitia blog yentu



                                         Sister Beata(Johari) akiwa on set

                      
                                          RAY Akiwa makini na kazi yake.


 
Huu mzigo si mchezo subirini kwa hamu sana, ni sinema niliyotumia hela nyingi sana mpaka kuona hivi watu walivyo....
     





                         Vijana wakipiga mzigo kwa umakini mkubwa sana.